Ufikiaji Salama na Huria wa Wickr

7/9/2018 - 1 dakika za kusoma

Imesasishwa: 26/10/2021

Psiphon inajivunia kutangaza ushirikiano mpya wa kusisimua. Katika miezi michache iliyopita tumekuwa tukifanya kazi na Wickr ili kuunda kipengele kipya cha majukwaa yao ya utumaji ujumbe salama:

Wickr: Secure Open Access.

Kupitia kipengele hiki, Wickr na Psiphon wamewezesha timu na biashara katika sehemu yoyote ya dunia — Marekani, Ulaya, Asia au Amerika ya Kusini — kupata huduma ya kutuma ujumbe uliosimbwa njia nzima (end-to-end), kupiga simu, kushiriki faili na skrini kwa uhakika bila kukatizwa kwa huduma. Hakuna jukwaa lingine la mawasiliano salama linalowezesha muunganisho usio na vizuizi popote duniani kwa njia hii.
Wickr, ambayo tayari imejikita vyema katika nyanja ya utumaji ujumbe salama kwa jukwaa lake thabiti, ilitambua kwamba kadiri mashirika yanavyozidi kuwa ya kimataifa, kunaweza kuwa na wasiwasi wa kiusalama pamoja na ule wa ufikiaji wakati wa kujaribu kuhakikisha mawasiliano salama kwa watu ulimwenguni kote.

Wickr inaamini watumiaji wao wa mwisho hawapaswi kuwa na wasiwasi kuhusu kuweza kuunganishwa na wenzao wa kazi, marafiki au familia - bila kujali mahali walipo, na Psiphon inakubaliana na hilo.

Kwa kuunganisha itifaki za mtandao za kisasa za Psiphon katika kipengele chao kipya, Wickr itawaruhusu watumiaji wao wa mwisho kulinda trafiki yao bila matatizo na kuituma kupitia mtandao wa Psiphon, kuhakikisha wanabaki wameunganishwa daima bila kujali mahali walipo.

Unaweza kusoma zaidi kuhusu ushirikiano wetu mpya hapa.
Habari za Kampuni

Soma inayofuata